Nomzamo Winifred Madikizela-Mandela, mke
wa zamani wa mpigania uhuru wa Afrika Kusini hayati Nelson Mandela
amefariki dunia dunia Jumatatu mchana akiwa na umri wa miaka 81.
Mwanamama anafahamika kwa jina la Winnie
Mandela akionyesha ujasiri wake hasa alivyosimama kidete kupambana
dhidi ya utawala wa makaburu kipindi chote wakati Mandela akiwa
amefungwa kifungo cha maisha katika gereza la Robben Island.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Zodwa Zwane na akasema familia ingetoa taarifa zaidi baadaye.
No comments:
Post a Comment