Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel
Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe amesema ameitwa kuhojiwa na
Idara ya Uhamiaji siku ya Jumatatu, Aprili 9, 2018.
Akizungumza lleo Jumamosi Aprili 7, 2018 Askofu Kakobe amesema ataitikia wito huo.
“Wamenieleza kuwa wananiita kwa sababu
ya mahojiano hivyo nitakwenda tu hakuna shida. Wameniita Uhamiaji mkoa
wa Dar es Salaam,”amesema Kakobe.
No comments:
Post a Comment