DODOMA
Mwanamziki wa nyimbo za Injili Stannely Charles,anatarajia kufanya uzinduzi
wa albam yake inayoitwa kwa jina la kifaranga cha kuku,utakaofanyika tarehe
29April 2018 katika kanisa la KTM Dodoma.
Akiongea na Gospel News ya Habari Maalum ya vyombo vya habari
bwana Stannely,amesema anamshukuru Mungu kwani maandizi ni mazuri.
Hivyo anawakaribisha watu wote katika uzinduzi huo
utakaofanyika katika kanisa la Healing cetre K.M.T Dodoma, sambamba na uzinduzi
wa albam ya kifaranga cha kuku amesema atazindua
albam yake ya pili ambayo ipo katika mfumo wa audio inaayoitwa kwa jina la Neno lako.
Stannely amesema
katika uzinduzi huo kutakuwa na wasanii
wengine wa nyimbo za injili watakaokuwepo ili kumuunga mkono ikiwa ni
pamoja na mwanamziki smart boy kutoka Dar es salaam,Daniel Mwanza pamoja na Luth
lameck kutoka Dodoma.
Hata hivyo Stannely ametoa shukrani kwa mashabiki wake kutoka
sehem mbalimbali,pia amewajuza kuwa zipo video zake nyingi YouTube ni pamoja na nyimbo ya umenitoa
mbali,nikimaliza kazi pamoja na albam yake ya pili anayotarajia kuiingiza hivi
punde.
No comments:
Post a Comment