Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa
Palamagamba Kabudi, amesema mawakili sita wamesimamishwa kufanya kazi ya
uwakili kwa miezi sita hadi miaka mitano kwa makosa ya nidhamu.
Kabudi ameyasema hayo leo bungeni wakati akiwasilisha mipango wa makadirio ya bajeti ya wizara ya Katiba na Sheria.
Amesema uamuzi huo umetolewa na kamati ya nidhamu ya mawakili baada ya kupokea malalamiko hayo
Profesa Kabudi, amesema kamati hiyo
ilipokea malalamiko 18 ya mawakili kwa mwaka wa fedha 2017/2018 na hivyo
kufanya jumla ya malalamiko yaliyokuwa mbele ya kamati kufikia 48.
“Katika kipindi hicho, malalamiko 22
yalisikilizwa na kutolewa uamuzi ambako mawakili sita wamesimamishwa
kazi ya kufanya uwakili kwa muda wa miezi sita hadi miaka mitano,”
amesema.
Ametoa wito kwa mawakili wote nchini
kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu wakitambua kuwa wao ni maofisa
wenye dhamana kubwa ya kufanikisha utoaji wa haki kwa wakati.
No comments:
Post a Comment