ASKARI Polisi waliokuwa lindoni katika Benki ya CRDB Tawi la Tanga Mjini wanadaiwa kupigana risasi Jumamosi, Aprili 14, 2018 na kusababisha kifo cha mwenzao mmoja, hata hivyo, majina yao hayajafahamika mara moja.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo,
inadaiwa kwamba, mmoja wa askari hao alimpiga risasi mwenzake na
kumjeruhi mguuni hivyo akawa kama amepagawa na kuanza kufyatua risasi
hovyo. Inadaiwa pia kwamba chanzo cha ugomvi huo ni tuhuma za wivu wa
mapenzi.
Wakati tukio hilo likitokea inadaiwa
askari wengine walikuwa eneo la jilani wakifanya mazoezi hivyo baada ya
kuona mtu akirusha risasi hovyo walihisi ni mhalifu hivyo wakamfyatulia
risasi iliyompata kichwani na kupoteza maisha.
Hata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Michael Wakulyamba
ambaye amesema hajatapata taarifa za tukio hilo kwani yupo safarini
hivyo anafuatilia ili kufahamu iwapo ni kweli limetokea na mazingira ya
tukio yalikuwaje.
No comments:
Post a Comment