Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kongwa
mkoani Dodoma, Mhandisi Ngusa Izengo anadaiwa kufariki dunia baada ya
gari lake kuangukiwa na lori la mafuta usiku wa kuamkia Aprili 15,
2018 katika eneo la Chalinze Nyama nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Giles Muroto alipokuwa anazungumza na
mwandishi wa habari hii na kusema atatoa taarifa kamili baada ya
kukamilisha.
"Nitatoa taarifa kamili zoezi hili
uokaji litakapomalizika maana mpaka muda huu tumetoka eneo la tukio
tumeshindwa kujua kuna watu wangapi ndani ya gari hilo lililoangukiwa.
Tunaenda TAMESA kutafuta 'grinder machine' ilituweze kujua idadi kamili
ya miili iliyopo ndani ya gari",amesema Kamanda Muroto.
No comments:
Post a Comment