Askofu Kiongozi wa Moravian Tanzania
jimbo la Kusini Magharibi Alinikisa Cheyo, amewaasa Watanzania kuacha
kulalamika na badala yake wajikite katika kufanya kazi njema
inayompendeza Mungu.
Askofu Cheyo ametoa kauli hiyo katika
ibada ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa Moravian Tanzania jimbo la
kusini Magharibi ushirika wa Mbeya Mjini.
Askofu amesema ili Watanzania waweze
kujiletea maendeleo yenye tija kufikia uchumi wa kati wanapaswa kuachana
na mambo ya kisiasaili waweze kufanya shughuli zao za kujiingizia
kipato.
Askofu Cheyo pia ametumia fursa hiyo
kuwaasa viongozi wake wengine wa dini nchini kutofautisha dini na siasa
ili kujenga upendo miongoni mwa Watanzania ikiwa ni pamoja na kudumisha
amani ya nchi.
No comments:
Post a Comment