Katika Kikao cha Bunge nchini Kosovo, wabunge wa upinzani wameingia na gesi za machozi bungeni.
Wabunge hao waliwasha gesi hizo na kuvuruga mkutano huo ambao ulikuwa
ukitaka kupiga kura kuhusu mpango wa ugawaji wa mipaka na Montenegro.
Inaelezwa kuwa walifungulia gesi hizo mara mbili kwa nyakati tofauti
pindi kura hiyo ilipotakiwa kuanza kupigwa. Ilibidi polisi waingie
bungeni humo na kuwatoa wabunge hao wa upinzani huku wabunge wawili
wakiwa wamejeruhiwa.
No comments:
Post a Comment