
Serikali ya Nigeria imethibitisha
kuwa wengi kati ya wanafunzi wa kike 110 waliokuwa wametekwa na kikundi cha
Boko Haram zaidi ya mwezi mmoja uliopita wameachiwa Jumatano asubuhi.
Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa wasichana hao
waliletwa katika mji wa Dapchi ulioko upande wa Kaskazini mwa Nigeria wa Jimbo
la Yobe baada ya wale waliokuwa wanawashikilia kuwarejesha katika msafara
ulioandamana na magari 9.
Ripoti za vyombo vya habari zimesema wasichana watano kati
ya hao walikufa wakati wakisafirishwa, lakini afisa wa serikali wa jimbo la
Yobe amesema hili bado halijaweza kuthibitishwa.
Vyanzo vya habari nchini Nigeria vimetoa habari kuwa wakazi
wa eneo la Dapchi walikuwa wanafurahia kuachiwa kwa watoto hao.
No comments:
Post a Comment