Watu wasiojulikana wamevunja kufuli na
kuingia ndani ya Kanisa la Baraka na Uzima (GRM) lililopo Mtaa wa
Kokehogoma Kata ya Turwa wilayani Tarime na kufanikiwa kuiba vitu vya
kanisa hilo vyenye thamani ya zaidi ya Sh1.7 milioni.
Mchugaji wa kanisa hilo, Ezekiel Ngurumo amesema tukio hilo limetokea
usiku wa kuamkia leo Jumatano Januari 10 ambapo waliibia viti 28, spika,
inveta na jenereta vitu vya thamani hiyo.
“Tulishtuka baada kufika alfajiri kanisani kwa ajili ya maombi kama
ilivyo desturi yetu ya kila siku na kukuta vitu hiyo vimeibwa,” amesema
Mchugaji Ngurumo.
Mchugaji Ngurumo alilaani kitendo hicho na kuwataka wananchi kubadilika
na kuwa na hofu ya Mungu kwani vitendo walivyofanya hakijamfurahisha
Mungu.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kokehogoma, Josephat Ndonge amesema alipata
taarifa za vitu kuibwa ndani ya kanisa hilo mapema leo Jumatano na
kuwataka wananchi kutoa taarifa pale watakaposikia vitu hivyo vikiuzwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/ Rorya, Henry Mwaibambe
alikiri kuwepo kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kutoa taarifa za
wahalifu hao.
No comments:
Post a Comment