Waandishi wa habari watano wilayani
Kahama mkoani Shinyanga wamefikishwa mahakamani wilayani Kahama kwa
makosa ya kujifanya maafisa usalama wa taifa kutoka ikulu na kujipatia
fedha shilingi Milioni 1 kutoka kwa mganga wa jadi Jane Mbeshi (46).
Waandishi wa habari wanne kati ya watano
ambao ni Paul Kayanda wa gazeti la Uhuru,Raymond Mihayo-
Habarileo,Shaban Njia – Jamboleo,Simon Dioniz – Radio Kwizera
wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Kahama leo Jumatano Januari
10,2018 nana George Maziku ambaye hajulikani anaandikia chombo gani anatafutwa.
Akisoma mashtaka mahakamani hapo leo asubuhi,Hakimu Kazi wa mahakama ya wilaya ya Kahama,Keneth Mutembei alisema washtakiwa hao walijifanya
maafisa wa usalama wa taifa kutoka Dar es
salaam,Kigoma,Kagera,Shinyanga na Kahama kisha kujipatia shilingi
1,000,000/- kutoka kwa mganga wa jadi Jane Mbeshi (46) mkazi wa
kitongoji cha Ng’wande kata ya Mwaluguli wilayani Kahama baada ya
kumtishia kuwa anapiga ramli chonganishi.
Alisema waandishi wa habari watatu ambao
ni Paul Kayanda,Shaban Njia na Dioniz Maziku walikamatwa jana Januari
9,2018 saa saba na nusu mchana na jeshi la polisi wakijifanya maafisa wa
usalama wa taifa na kujipatia fedha kutoka kwa mganga wa jadi Jane
Mbeshi.
Hakimu huyo alisema walikamatwa baada ya
kuwekewa mtego kwani waliahidiwa fedha zingine tena shilingi milioni
1,000,000/- na mganga huyo wa jadi ambaye pia ni mkandarasi baada ya
kuchukua shilingi milioni 1 tarehe 6.1.2018 wakiwa na waandishi wa
habari wengine ambao ni Raymond Mihayo aliyekamatwa jana usiku saa nne
akiwa nyumbani kwake,na George Maziku ambaye bado anatafutwa kutokana na
kutojulikana alipo.
Mara baada ya kusoma mashtaka
hayo,hakimu huyo alisema dhamana ipo wazi kwa washtakiwa ambapo walikana
mashtaka hayo walikana kutenda makosa hayo.
Washtakiwa walirudishwa gerezani baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
No comments:
Post a Comment