\Serikali ya Botswana imelifunga kanisa la muhibiri mmoja wa Malawi mwenye utata anayedaiwa ''kutembea angani''.
Serikali ilithibitisha kufungwa kwa
kanisa la Bushiri la Christian Gathering Church ECG mjini Gaborone mara
kadhaa kutokana na wasiwasi kuhusu ''fedha za miujiza''.
Chombo cha habari cha Malawi24
kimeripoti kwamba kanisa hilo lilipinga uamuzi huo mahakamani
uliochukuliwa chini ya mwaka mmoja baada ya muhibiri huyo kupigwa
marufuku kuingia nchini humo.
Alikuwa ametarajiwa kuhudhuria kongamano fulani.
Mhubiri Bushiri wa kanisa la Christian Gathering Church ECG mjini Gaborone
Hata hivyo waziri wa Botswana Edwin
Batshu alitangaza mnamo mwezi Aprili 2017 kwamba bwana Bashir ambaye
sasa anaishi Afrika Kusini atahitaji Visa ili kuingia, licha ya raia wa
Malawi kutohitaji kibali hicho kulingana na chombo cha habari cha
AllAfrica.com
Serikali imetangaza kwamba kanisa hilo
litafungwa kabisa, huku gazeti hilo la Botwana likipata barua ilioambia
usimamizi wake kwamba kibali cha kuendesha kanisa hilo kimefutiliwa
mbali.
Gazeti hilo limeongezea kwamba ni hatua ya kanisa hilo kutumia ''fedha za miujiza'' ambayo imevunja sheria za taifa hilo.
Bwana Bushiri ambaye ana zaidi ya
''likes'' milioni 2.3 katika mtandao wa facebook na ambaye alivutia
umati mkubwa wa kuweza kujaza uwanja wa FNB mkesha wa mwaka mpya bado
hajatoa tamko lolote.
Kanisa hilo ni maarufu kwa mtindo wake
wa maisha ya kifahari kutokana na ufanisi wake ambao umevutia wafuasi
wengi barani Afrika.
Alishutumiwa mwaka uliopita baada ya
kubainika alikuwa akiwatoza kati ya dola 80 hadi 2000 wafuasi wake
waliotaka kuhudhuria chakula cha jioni naye kulingana na chombo cha
habari cha Afrika Kusini South Africa News24.
No comments:
Post a Comment