Jeshi la Polisi mkoani Mwanza
linawashikilia watu sita akiwemo Ofisa Ardhi wa Manispaa ya Ilemela,
Alex Nyabange (30), kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo utapeli wa viwanja,
kutengeneza vyeti bandia vya kitaaluma pamoja namba za mlipa kodi za
(TIN), za Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA).
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Alhamisi, Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema watu hao walikamatwa kwa
nyakati tofauti kati ya Desemba 30, 2017 na Janauari 9 mwaka huu.
Msangi aliwataja waliokamatwa kwa tuhuma za kuwatapeli watu kwa madai ya
kuwauzia viwanja kuwa ni Aloyce Nyabange (30) ambaye ni ofisa Ardhi wa
Manispaa ya Ilemela, Alex Josephat(41) ambaye ni mfanyabishara, Juma
Malulu (60) mkazi wa mta wa Ilemela.
Wengini ni Katibu Mhatasi wa kampuni ya Nyambale Civil Works, Getruda
Peter (42) mkazi wa Nyegezi na mchora ramani Deodatus Bety (51) mkazi wa
Usagara ambao wote walikamatwa Desemba 30, 2017 kwa nyakati tofauti.
“Tulipata taarifa hizi baada ya mtu mmoja ajulikanaye kwa jina la
Barnabasi Ibengo (39) mfanyabishara wa Kiseke kuwa ametapeliwa na watu
waliosema wana viwanja viwili eneo la Nyasaka na kwamba vinahitaji Sh45
milioni, lakini akawa ametanguliza Sh10 milioni akiamini kuwa ni ukweli
kutokana na nyaraka zote walizomuonyesha,” amesema Msangi.
Hata hivyo Msagi amesema mfanyabishara huyo, aligundua kuwa ametapeliwa
baada ya kwenda eneo vilipo viwanja hivyo na kuonana na mwenyekiti wa
mtaa huo na kuaambiwa hakuna jambo la namna hiyo ndipo alitoa taarifa
polisi na kuanza kufuatilia kukamatwa mmoja baada ya mwingine.
Alisema watuhumiwa hao walikutwa na komputa inayotumika kutengenezea
nyaraka mbalimbali na baadhi ya nyaraka zinazoonyesha viwanja kwa ajili
ya kuuzwa.
Kuhusu vyeti feki Kamanda Msangi amesema walimkamata Evancy Wilson (33)
katika mtaa wa Buzuruga Ilemela akiwa na vifaa vya kughushi vyeti vya
taaluma mbalimbali.
Amesema tukio hilo lilitokea Janauri 9, mwaka huu saa 11:00 jioni ambapo
mtuhumiwa baada ya kukamatwa na kuchunguzwa kwenye kompyuta yake
walikuta namba inayofanana na TIN ya TRA na vyeti hivyo vya taaluma vya
kughushi.
Amesema walikuta vyeti vya kughushi vya, stashahada, shahada, vyeti,
vitambulisho vya mpigakura, nyaraka zinazoonyesha kuwa ni za kuombea
mikopo benki, leseni za biashara na flash ambazo zimejazwa vitu hivyo.
“Hili lilitokana na taarifa tulizopata kutoka kwa raia wema kuhusu
kuwapo kwa mtu anayetenegeza vitu hivyo ndipo tulianza kufuataili,
watuhumiwa wote wapo polisi, upelelezi ukikamilika tutawafakisha
mahakamani.
No comments:
Post a Comment