Benchi
la Ufundi la Majimaji FC, limesema kuwa, kukosekana kwa nyota wake
wanne kwenye mchezo wao wa juzi Jumamosi dhidi ya Mtibwa Sugar, ndiyo
sababu kubwa iliyowafanya washindwe kupata matokeo mazuri na kuambulia
kipigo.
Juzi
Jumamosi kwenye Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro, Majimaji
inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya Sokabet, ilifungwa
mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Ofisa
Habari wa Majimaji, Onesmo Ndunguru, alisema nyota hao ambao ni Seleman
Selembe, Paul Mahona, Tumba Sued na Abdallah Salamba, hawakuwepo
kutokana na matatizo mbalimbali.
“Kama
wangekuwepo nyota wetu wote nadhani tungeweza kuibuka na ushindi,
lakini kukosekana kwao kumesababisha tupate matokeo hayo mabaya.
“Kikubwa
tunajipanga kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye michezo yetu ijayo ili
tuweze kuwa sehemu salama ambapo mwisho wa msimu tubakie kwenye ligi,”
alisema Ndunguru.
No comments:
Post a Comment