Imani potofu kama vile kulogwa zimeripotiwa kuwa ni kikwazo
katika kutibu ugonjwa wa Ukoma wakati huu ambapo visa vipya 200,000 vya ukoma
huripotiwa kila mwaka. Ni kutokana na hali hiyo katika maadhimisho ya
siku ya Ukoma duniani tarehe 28 mwezi huu, Umoja wa Mataifa unataka hatua
zichukuliwe na serikali zihakikishe zinatokomeza unyanyapaa dhidi ya wagonjwa.
Taarifa zaidi na John Kibego.
Huyu ni Rowin Luvanda, mtanzania ambaye ni mgonjwa wa Ukoma,
ugonjwa unaoenezwa na vimelea kwa njia ya hewa lakini kwa miaka mitatu alisaka
tiba hadi za kienyeji ambako alielezwa kuwa..
Umoja wa Mataifa umetaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 22
ambamo kila mwaka kuna visa vipya vya wagonjwa ambapo Rowin baada ya kuhangaika
miaka 3 hatimaye alikwenda hospitali ya Lugalo jijini Dar es salaam.
Kufuatia mahangaiko ya Rowin hadi kupata huduma sahihi baada
ya miaka mitatu, tumemuuliza Meneja wa mpango wa Taifa wa kutokomeza
Kifua Kikuu na Ukoma nchini Tanzania Dkt. Beatrice Mutayoba je tiba ya ukoma
inapatikana wapi?
Nchini Tanzania visa vipya ya ukoma bado vinaripotiwa Lindi,
Rukwa, Mtwara, Morogoro, Pwani; Tanga, Geita, Dodoma, Tabora na Kigoma.
No comments:
Post a Comment