Mtu mmoja anaye jiita Nabii Tito ambaye kwa sasa anashikiliwa na jeshi la Polisi Mkoani Dodoma amejikata na viwembe sehemu ya tumbo, na kupata majeraha yaliyopelekea klukimbizwa hospitali.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Giles Muroto, amesema tukio hilo limetokea wakati walipoenda kufanya upekuzi nyumbani kwake, na ndipo alipopata mwanya wa kufanya hivyo kwa kutumia viwembe vilivyokuwa chini ya godoro.
“Alijikata wakati tunafanya upekuzi nyumbani kwake kupata vielelezo vinavyohusiana na matukio yake, aliomba kukaa chini, alivyotaka kukaa chini kumbe chini ya godoro kulikuwa na viwembe akavichukua ghafla bila kutegemea alijikata tumboni, amepata majeraha mpaka ile ngozi ya ndani ndogo, lakini polisi waliwahi kumdhibiti na kumpeleka hospitali, kapatiwa matibabu na kurudishwa”, amesema Kamanda Muroto.
Kamanda Muroto amesema kwa sasa Nabii Tito amesharudishwa kituoni na yuko salama, na wanatarajia kumfikisha mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.
No comments:
Post a Comment