Rais wa
Marekani Donald Trump ameendelea na msimamo wake wa kutishia kusitisha
misaada kwa Taifa la Palestina endapo litakataa kushiriki kwenye
mazungumzo ya amani.
Wizara ya
Masuala ya Kigeni Marekani imethibitisha kwamba Trump alitoa msimamo huo
alipokuwa akizungumzia kuhusu msaada wa kiuchumi na usaidizi wa
kiusalama, ambapo aliituhumu Palestina kulivunjia heshima Taifa lake.
Msimamo huo
umekuja ikiwa zimepita siku kadhaa tangu nchi ya Marekani kuzuia fedha
kiasi cha dola milioni 65 zilizopangwa kwa ajili ya kulisaidia Shirika
la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi wa Palestina.
Hivi karibuni
Palestina imeikataa Marekani kuwa mpatanishi asiyependelea upande
wowote katika mazungumzo ya amani, kufuatia hatua ya Marekani kuutambua
mji wa Yerusalem kama mji mkuu wa Israel.
No comments:
Post a Comment