Vatican imesema Papa Francis atatembelea taifa la Lithuania,
Latvia na Estonia mnamo Septemba 22-25 yakiwa ni mataifa matatu ya Baltic
yanayosherehekea maadhimisho ya miaka 100 ya umoja wao.
Vatican imethibitisha safari hiyo Ijumaa ya wiki iliyopita, wakisema Papa Francis atatembelea mji wa Vilnius na Kaunas huko Lithuania; Riga na Aglona huko Latvia, na Tallinn huko Estonia.
Lithuania ina jumuiya kubwa ya Kikatoliki katika mataifa ya
Baltics, ikiwa na zaidi ya asilimia 75 ya wakazi wa nchi hizo ambayo sawa na
karibu watu milioni 3.
Mataifa hayo matatu ya Baltic yalitangaza uhuru wao kutoka
kwenye mikono ya Urusi mwaka wa 1918 lakini yaliingizwa katika Umoja wa Sovieti
mwaka wa 1940 na ikawa sehemu yake mpaka 1991.
Kwa nafasi iliyobaki kwa mwaka 2018 Papa Francis ana safari
nyingine moja tu iliyothibitishwa ambayo ni safari ya kuelekea Geneva mwezi
Juni. Pia anatarajia kwenda Ireland mwezi Agosti kwa Mkutano wa Dunia unaohusu
Familia.
No comments:
Post a Comment