Rais John Magufuli amesema Serikali ina mpango wa kufuta utitiri wa mifuko ya hifadhi ya jamii na kubakiza miwili.
Amesema mifuko itakayobaki ni kwa ajili ya kuhudumia wafanyakazi wa sekta binafsi na ya umma.
Rais Magufuli amesema Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
litabaki kwa ajili ya kuhudumia wafanyakazi wa sekta binafsi wakati
mifuko mingine yote itaunganishwa na kuwa mmoja.
Amesema hayo jana Alhamisi Desemba 14,2017 alipofungua mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) mjini Dodoma.
Mifuko mingine inayotoa huduma ya hifadhi ya jamii ni PSPF, LAPF, PPF na GEPF.
Rais Magufuli alisema baadhi ya mifuko ya hifadhi ya jamii imekuwa
haiwasaidii wafanyakazi badala yake imekuwa ikiwekeza kwenye ujenzi wa
majengo makubwa.
“Mifuko hii haiwanufaishi wafanyakazi bali wapiga dili ambao huamua majengo yajengwe na wao kupata asilimia 10,” alisema.
No comments:
Post a Comment