
MWALIMU wa Shule ya msingi, Itiryo
tarafa ya Ingwe wilayani Tarime mkoani Mara, Samwel Mariba Daniel (29)
amefikishwa katika mahakama ya wilaya Tarime akituhumiwa kuwabaka
wanafunzi wake tisa wenye umri wa chini ya miaka 10 kwa nyakati tofauti
kuanzia mwezi Agosti na Novemba mwaka huu.
Akisomewa mashitaka hayo ya ubakaji
katika kesi ya jinai namba 682/2017 mbele ya Hakimu wa Mahakama ya
Wilaya Tarime, Amon Kahimba, Mwendesha Mashitaka wa Polisi Inspekta
Saumu Ngoma alidai kuwa mtuhumiwa Mariba alitenda makosa hayo kati ya
ubakaji kwa nyakati tofauti kwa wanafunzi wake wa darasa la kwanza na la
pili kati ya Agosti na Novemba mwaka huu 2017.
Mwendesha mashitaka alidai kuwa,
wanafunzi hao wa kike chini ya miaka 10 ambao majina yamehifadhiwa
walibakwa na mwalimu huyo kwa nyakati tofauti wakati wakiwa maeneo ya
shule hiyo kwenye nyumba za walimu.
Alidai mwalimu alikuwa akiwatuma na kisha wanapokuwa ndani ya nyumba alikuwa akitenda kosa hilo.
Chanzo- Habarileo
Alidai mwalimu alikuwa akiwatuma na kisha wanapokuwa ndani ya nyumba alikuwa akitenda kosa hilo.
Chanzo- Habarileo
No comments:
Post a Comment