Manchester United wameulizia kumhusu kiungo wa kati wa Chelsea na Brazil Willian, 29. (Daily Mail)
Meneja
wa United Jose Mourinho pia yuko tayari kumuuza kiungo wa kati wa
Armenia Henrikh Mkhitaryan, 28, majira ya joto na anataka kumnunua
kiungo wa Arsenal na Ujerumani Mesut Ozil, 29, kujaza nafasi yake.
(Daily Mirror)Chelsea nao huenda wakamtumia mshambuliaji wa Belgium Michy Batshuayi, 24, kama kikolezo kwenye mkataba wa kumchukua winga wa Monaco na Ufaransa Thomas Lemar, 22, ambaye amekuwa pia akitafutwa na Liverpool na Arsenal.(Sun)
Kiungo wa kati wa Bayern Munich na Ureno Renato Sanches, 20, huenda akarejea kwa klabu yake mapema kutoka kwa mkopo Swansea Januari. (Mais Futebol)
No comments:
Post a Comment