Mfanyabiashara mmoja nchini Japan ambaye anaugua saratani na anatarajiwa
kufariki karibuni amewashangaza watu baada ya kuandaa karamu kubwa ya
kuaga.
Satoru Anzaki aliwaalika wageni karibu 1,000 wakiwemo marafiki zake,
watu waliosoma naye, washirika wake wa kibiashara na wafanyakazi wake.
Satoru, 80, ambaye ni mkuu wa zamani wa kampuni ya kuunda mashine ya
Komatsu alipatikana na saratani ya kibofu cha nyongo Oktoba.
"Nimeridhika kwamba niliweza kusema 'asante' kwa watu niliokutana nao maishani," aliwaambia wanahabari baada ya sherehe hiyo.
"Kwa kuwa nilitaka kufurahia kabisa sehemu ndogo ya maisha niliyobaki
nayo, nimeamua nisipokee matibabu baada ya kuzingatia madhara ya tiba,"
alisema.
Alitangaza mpango wake wa kufanya sherehe hiyo kupitia tangazo gazetini,
taarifa ambazo zilisambazwa sana mtandaoni watu wakitaniana kuhusu
ingelikuwa wao wangewaalika nani.
Satoru alikodisha chumba katika hoteli moja Tokyo na akaipamba kwa picha za kumbukumbu ya maisha yake.
Chanzo- BBC
No comments:
Post a Comment