Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis ameruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Gemelli, Roma nchini Italia alikokuwa akitibiwa, zikiwa ni siku 11 tangu alipofanyiwa upasuaji wa kuondoa sehemu ya utumbo wake.

Papa Francis ametoka hospitalini hapo kimyakimya kwa kutumia mlango mdogo kisha akaingia kwenye gari lake la kawaida, akisindikizwa na msafara mdogo uliojumuisha maafisa kutoka Vatican na maafisa usalama wa Italia ambapo sasa, atakuwa kwenye mapumziko ya nyumbani kwa muda usiopungua wiki mbili.

Taarifa zake za kutolewa hospitali, hazikutangazwa mapema mpaka alipowasili Vatican, makao makuu ya Kanisa Katoliki Duniani ambapo baada ya kuwasili, ameongoza misa maalum katika Kanisa la Rome Basilica of Santa Maria Maggiore akionesha kuwa mwenye afya njema.

Ni kawaida kwa Papa Francis kuendesha misa katika kanisa hilo kila anaporejea Vatican kutoka kwenye ziara za nje na lengo la misa hiyo huwa ni kumshukuru Mungu kwa kumrejesha salama.

Jumapili iliyopita, Papa Francis akiwa katika Hospitali ya Gemelli inayoendeshwa na Kanisa Katoliki Duniani, alijitokeza hadharani kwa mara ya kwanza, kwa kusimama juu ya kiambaza cha wodi aliyokuwa amelazwa, na kuongoza misa ya Jumapili huku akiwa amesimama mwenyewe bila msaada kwa takribani dakika kumi.

Kwa mujibu wa Vatican, Papa Francis alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa ambao kitaalamu huitwa symptomatic diverticular stenosis (Simptomatiki Daivetikyula Stenosisi) ambao ulikuwa umeshambulia sehemu ya utumbo wake mkubwa na kutengeneza uvimbe tumboni.

Madaktari walilazimika kumfanyia upasuaji wa kuondoa sehemu ya utumbo wake mkubwa uliokuwa umepata madhara katika oparesheni ambayo ilifanyika kwa mafanikio makubwa.

Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Papa Francis kulazwa hospitali tangu mwaka 2013 alipochaguliwa kushika wadhifa huo mkubwa zaidi katika Kanisa Katoliki.

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba Papa Francis atarejea kwenye majukumu yake ya kawaida kuanzia Agosti 4, mwaka huu ambapo pia anatarajiwa kufanya ziara katika nchi za Slovakia na Hungary katikati ya mwenzi Septemba.  Imeandaliwa na Hashim Aziz kwa msaada wa mitandao.

PAPA FRANCIS ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITAL

No comments:

Post a Comment