Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Kutoka Arusha ambaye pia ni Producer na Mtunzi wa Gospel Erasto Mwashinga amesema Morden Gospel haijapunguza wala Kuongeza Ubora na Ladha ya Kusikilizwa zaidi na Watu wengi.
Erasto Mwashinga amezungumza Hayo wakati akihojiwa na Mtangazaji wa Kipindi cha Gosple Climax ya habari Maalum tv Method Charles ambacho huwa kinapeperushwa Kila Jumamosi Usiku kupitia Youtube Chaneli ya Habari Maalum Tv.
“ Kwenye Morden Gospel wamejikita kwenye kuboresha Muziki uwe rahisi zaidi na watu waupende lakini bado haijaongeza kundi la watu kuusikiliza zaidi wala Kupunguza watu kuusikiliza”Alisema Erasto Mwashinga Mwimbaji, Producer na Mtunzi wa Gospel Kanda ya Kaskazini.
Aidha amebainisha kuwa kumekuwa na watu Baadhi ambao wamepokea Vizuri Morden Gospel Lakini kuna wengine ambao ukichezwa wanajaribu kufananisha na Muziki wa Kidunia jambo ambalo linakuwa sio zuri.
“Mordern gosppel Inapendwa zaidi Maeneo ya Mjini lakini ukienda Vijijini sio rahisi sana Kuona Watu wanapenda huu Muziki wa Morden Gospel wanapende Ladha ya Muziki wa injili wa zamani”
Hata Hivyo amewataka waimbaji Kujikita zaidi Kuimba Nyimbo za Kumtukuza Mungu na Kumsikiliza Roho Mtakatifu kwanza Kabla ya kufa maamuzi katika Kutoa Nyimbo.
Erasto Mwashinga anamiliki Studio yake Iitwayo EM STUDIO Kijenge Mkoani Arusha na katika Kazi yake ya Kuandaa Muziki amewahi kuwaaandalia waimbaji mbalimbali ambao kwa sasa wanafanya Vizuri katika Gospel Kama vile Doreen Tito, Malaki Mbise, Imani Mwasambapa na wengine.
CHANZO CHA HABARI
Mwimbaji | Mtunzi : Erasto Mwashinga
Contact : +255692401260
Kanisa : TAG BETHEL KIJENGE ARUSHA
No comments:
Post a Comment