By Nasra Abdalah
Msanii wa muziki wa Bongofleva,Faustina Charles, maarufu Nandy ameachia kwa mara ya kwanza video ya wimbo wake wa Injili.
Wimbo
huo unaoitwa ‘Wanibariki’, ameuachia leo Jumatatu Aprili 5,2021,
katika youtube yake, ambapo mpaka sasa umeshatazamwa na watu zaidi ya
100,000.
Machi mwaka huu, msanii huyo aliyefikisha watazamaji
milioni moja kwenye mtandao wa Youtube, alitekeleza ahadi yake ya
kuachia EP ya nyimbo za Injili, kama ambavyo aliwahi kuwaahidi
mashabiki zake huko nyuma.
EP hiyo ina jumla ya nyimbo tano,ukiachilia mbali Wanibariki, Ipo Umenifaa,Nipo Naye, Asante na Noel ya Kwanza.
Wanibariki ndio utakuwa wimbo wa kwanza kuachiwa video yake katika EP hiyo.
Nandy
aliyeanza kuvuma miaka minne iliyopita na kibao chake cha Nagusagusa,
amekuwa moto wa kuotea mbali na kuwa moja ya wasanii wa kike wanaofanya
vizuri kwa sasa.
Vibao kama Kivuruge,
Ninogeshe,Wasikudanganye, Na Nusu vilizidi kumuweka kwenye ramani nzuri
ya soko la muziki na kujikuta akipata tuzo mbalimbali za nje ya nchi na
kufanya kazi na wasanii wakubwa akiwemo Koffi Olomide wa DRC Congo, Joe
Boy wa nchini Nigeria, Saut Soul na Willy Paul wa Kenya.
No comments:
Post a Comment