Na Method Chaz
Taasisi isiyo ya kiserikali Blue Cross Society Tanzania imefanikiwa kutoa elimu ya Matumizi ya pombe na dawa za kulevya kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Ngarenaro iliyopo Arusha mjini.
Elimu hiyo inayotolewa kwa vijana walio katika umri kuanzia miaka 12 hadi 17 pamoja na wananchi ambao wanapatikana katika maeneo ya Mkoa wa Arusha ambayo wameyatenga kwaajili kutoa Elimu ya jinsi ya Kupambana na Madawa ya Kulevya na Pombe.
Akizungumza na Habari Maalum Media Meneja wa Mradi wa Blue cross Society Tanzania Anna Panga amesema "Tumeweza kutumia dakika 40 kwaajili ya kuwafundisha vijana namna ya kusema hapana katika matumizi ya pombe na dawa za kulevya na pia kuepuka katika kundi Rika”Alisema Anna Panga.
Aidha kwa upande wa Wanafunzi katika shule hiyo wameeleza Jinsi gani walivyo jifunza kutokana na elimu hiyo walio ipata na watakavyo elimisha jamii inayo wazunguka kwa kutumia elimu waliyo ipata kutoka Blue Cross Society Tanzania.
Anisha Fadhili ni Mwanafunzi katika Shule ya Msingi Ngarenaro anasema kuwa atatoa elimu kwa vijana ili kuhakikisha kuwa wanaepukana na Madawa ya Kulevya ikiwa ni pamoja na Jamii inayo mzunguka.
Amesema alicho jifunza ataenda kukifanyia kazi kwa kuwapa wenzake elimu kuhusu madawa ya kulevya ni mabaya kwasababu yanaweza kukusababisha kuacha shule na kupata magonjwa mbali mbali ikiwemo ukimwi.
Iddy Asenga mwanafunzi wa kidato cha kwanza amesema atatoa elimu kwa wanajamii mbalimbali na blue cross imewasaidia kuwapa elimu kuhusu madawa ya kulevya hivyo wata wasaidia jamii kwa kuwapa elimu jinsi ya kujikinga na madawa ya kulevya.
Hata hivyo Mwalimu wa shule hiyo Mwal. Mtei ameeleza kuwa Wanafunzi wa SHule hio wamefaidika na elimu hiyo inayotolewa na Blue Cross Society Tanzania juu ya maswala ya matumizi ya pombe na dawa za kulevya na namna ambavyo wanafunzi wata elimisha jamii inayo wazunguka.
CHANZO CHA HABARI
BLUE CROSS SOCIETY TANZANIA
CONTACT : +255757209441
MAHALI : ARUSHA TANZANIA
No comments:
Post a Comment