Baada ya tangazo la Papa, askofu mkuu Kambanda ameiambia runinga ya taifa ya Rwanda kuwa “hiki ni kitu ambacho hata sikuwahi kufikiria kwamba kinaweza kutokea”.
Askofu mkuu Kambanda ndio kadinali pekee wa Afrika aliyetajwa miongoni mwa makadinali 13, ambao watatawazwa katika sherehe itakayofanyika Vatican Novemba 28.
Rwanda, nchi yenye idadi kubwa ya waumini wa Kikatoliki inaungana na Kenya, Uganda na Tanzania, kama nchi za Afrika Mashariki kuwa na makadinali hivi karibuni.
Kati ya idadi ya makadinali 219 kote duniani sasa hivi, 29 pekee ndio wanaotoka Afrika.
CHANZO CHA HABARI
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment