TAMASHA LA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI KUOMBEA UCHAGUZI MKUU LAAHIRISHWA


 

 

Tamasha la waimba wa injili lililoandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion na kwa ajili ya kuuombea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu limeahirishwa mpaka hapo litakapotajwa tena.

Tamasha hilo lilitakiwa kufanyika septemba 6 mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwa leo Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama amesema tamasha hilo limeahirishwa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake.

Akitaja baadhi ya sababu hizo Msama alisema ni kuambiwa wakitaka kufanya tamasha hilo limalizike saa kumi na mbili jioni muda ambao tamasha lingekuwa limeanza kunoga.

Hata hivyo sababu hiyo na nyinginezo ndizo zilizosababisha kuahirishwa kiwa tamasha hilo.

 

No comments:

Post a Comment