Mwimbaji wa Nimbo za Injili Nchini toka Nyanda za Kaskazini Ezekiel Maasai amesema aliwahi kurudishwa na Muandaaji wake wa Muziki kwenda kujifunza Upya.
Akizungumza katika Kipindi cha Gospel Climax Kinacho Tazamwa kupitia You tube Channel ya Habari Maalum Media Ezekiel amesema wito wa Kuimba ulimjia baada a Mungu kumuokoa katika Utumiaji wa Madawa ya Kulevya aina ya Bangi.
Amesema Siku ya Kwanza kuingia Studio kurekodi alianza Mazoezi kama kawaida licha ya kuona yeye yupo sahihi katika Uimbaji lakini alikuwa anakosea hali ambayo ilimfanya Muandaji wake wa Muziki Kumrudisha Akajifunze upya kuimba.
Maasai amesema kuwa anatarajiia Kuzindua Video yake Mpya ambayo inakwenda kwa jina la Yesu amenilipia Deni ambayo imeandaliwa na wadhamini wake aliowapata Baada ya Kushinda Katika shindano la NIUWEZA TV lililokuwa na Lengo la Kuwatangaza Waimbaji wa nimbo za Injili.
Katika Shindano hilo wimbo wake ulishinda kwa Kutazamwa na watu wengi Zaidi kupitia Youtube Channel Hiyo.
Uzinduzi wa Video hiyo utafanyika Katika Kanisa la Sauti ya Nabii Niuweza wa Mungu lililopo Muriet Dampo Mkoani Arusha.
Hata Hivyo Ezekiel amewaomba wadau Mbalimbali wa Muziki Kujitokeza Kwa Wingi katika Uzinduzi wa Video yake amabayo ameitengeneza Kwa Viwango Bora Kabisa.
No comments:
Post a Comment