Waumini wa kanisa la Jubilee Christian Church (JCC) huko nchini Kenya
wamejikuta wakigawanyika makundi mawili mara baada ya askofu wao kutaja
ujio wa mgeni ulioleta utata na gumzo kubwa miongoni mwa wauamini hao.
Mgawanyiko huo ulitokea mara baada ya Askofu Allan na mchungaji Kathy
Kiuna kumkaribisha mwandishi wa habari kutoka CNN, Richard Quest
aliyefunguka na kuweka wazi kuwa ni shoga.
Mualiko huo waliutangazwa kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter
ukidai kuwa mwanahabari huyo atajumuika pamoja na waumini wa JCC katika
misa ya jumapili ijayo.
Wapo waliosema kitendo cha kumkaribisha shoga huyo kanisani ni sawa
na kuunga mkono biashara ya ushoga inayofanywa na mwandishi huyo, lakini
pia wapo walisema tunaishi katika dunia huru hivyo haitakiwi
kuhukumiana.
Quest kwa mara ya kwanza alifunguka juu ya kuwa shoga mwaka 2014, na
kusema kuwa yeye kuwa shoga haiathiri biashara na kazi yake ya uandishi
wa habari.
Alipofanyiwa mahojiano na kituo cha radio cha Capital FM jana asubuhi
alipinga vikali kitendo cha wakenya kuwachukulia tofauti watu wenye
mapenzi ya jinsia moja na kusema watu hao wanapaswa kufanya shughuli zao
wakiwa huru.
Ameongezea kuwa ili Kenya iwe nchi yenye maendeleo inabidi iwaache
watu waishi watakavyo na kuwapenda kwa vile walivyochagua kuwa na kwa
kile wanachotaka kukifanya.
Hata hivyo nchi zote za Africa zinapinga vikali ikiwa ni pamoja na kutounga mkono harakati za mapenzi ya jinsia moja.
No comments:
Post a Comment