Sheria
mpya ambayo inafanya unyanyasaji wa kingono na Udhalilishaji kuwa ni
Uhalifu itaanza kutekelezwa nchini Morocco hivi karibuni.
Sheria
hiyo ambayo inajumuisha upigaji marufuku wa ndoa za kulazimishwa,
inafuatia kuongezeka kwa hali ya wasiwasi katika miaka ya hivi karibuni
juu ya kiwango cha udhalilishaji wanawake.
Utafiti mmoja uliofanywa nchini humo, umeonesha kuwa wanawake sita kati ya 10 nchini Moroccan wamepitia manyanyaso hayo.
Matukio ya ubakaji ya hivi karibuni yametangazwa sana katika mitandao ya kijamiii.
Mwandishi wav BBC mjini Rabat amesema sheria hiyo mpya
imepokelewa vizuri lakini pia imekosolewa kwa sababu haitoi maana kamili
ya unyanyasaji majumbani au marufuku katika vitendo vya ubakaji ndani
ya ndoa.
Kwa mujibu wa sheria hiyo, wale wote watakaotiwa hatiani
kwa makosa ya kudhalilisha kingono hadharani iwe kwa kutumia maneno, ama
ishara yoyote ya kudhalilisha kijinsia atakabiliwa na hukumu ya kifungo
kuanzia mwezi mmoja mpaka sita gerezani na pia faini ya fedha taslimu
Mashirika ya haki za binadamu yanasema kuwa wanawake wengi nchini Morocco wamekuwa ni wahanga wa matukio ya unyanyasaji kingono.
Katika
ripoti yake ya mwaka 2015, Shirika la Haki za Binadamu nchini humo
limearifu kuwa zaidi ya asilimia 20 ya wanawake nchini Morocco
wamekumbwa na matukio ya unyanyasaji wa kingono japo mara moja katika
maisha yao
Katika siku za hivi karibuni polisi nchini humo
iliwakamata vijana 12 kwa tuhuma za kumbaka msichana wa miaka 17 na
kumtesa katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.
No comments:
Post a Comment