Mwanaume mmoja kwa jina Jonas Moses 52 amemuua mwanawe wa
kiume Moses Jonas17 kwa kumkatakata na panga sehemu za kichwa katika kitongaji
cha Ekenywa kata ya olturumeti na kumtupa kitongoji cha Ekyushini wilaya ya
Arumeru mkoani Arusha usiku wa kuamkia Jumamosi.
Akizungumza na Habari Maalum Fm Mwenyekiti mstaafu wa
kitongoji cha Ekyushin William Samuel Kalama amsema chanzo cha mwanaume huyo
kutekeleza mauaji hayo ni ugomvi uliopo baina yake na mzazi mwenzake sababu
ikiwa hakutaka mwanae wakiume akatairiwe kwa ukoo wa wajomba.
Nao baadhi ya wanachi wa eneo hilo wameeleza kusikitishwa na
kitendo hicho cha kinyama na kueleza jinsi walivyoiona hali hiyo baada ya
kitendo hicho kutokeo asubuhi ya leo walipokuwa katika shuhuli zao.
Hatahivyo Kalama ametoa wito kwa
serekali kutoa adhabu kali kwa mhusika
ili kuhakisha kwamba linakuwa funzo kwa jamii kwani baadhi ya watu
wanaotekeleza unyama huu wameonekana kutojali hata wanapoachiwa huru na hivyo
amesisitiza adhabu itolewe ili kuhakikisha vitendo hivi vinadhibitiwa.
No comments:
Post a Comment