Zaidi ya Wananchi 100 wa kijiji cha Msitu wa Tembo Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara hawana mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kuanguka na kusombwa na mafuriko ikiwemo ya mwenyekiti wa kijiji.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Bw Abel Mfuru amesema, zaidi ya nyumba 20 za udongo pamoja na vyoo vyake vimesombwa na mafuriko hayo na wananchi hakuna walichookoa katika nyumba hizo vikiwemo vyakula na nguo.
Bw .Mfuru amesema mvua hiyo ilianza kunyesha saa mbili za usiku na kuambatana na radi kali zaidi ya nne ambazo hata hivyo pamoja na mafuriko hayo hakuna aliyejeruhiwa.
Wananchi walioathiriwa na mafuriko
hayo Bi. Maryana Hussein na Bw Paul Yohana ambayo yamesababishwa pia na
kukatika kwa korongo moja ambalo lilizidiwa na maji wameiomba serikali msaada
wa haraka wa chakula, mavazi na dawa.
Afisa Mtendaji wa kata ya Msitu wa Tembo Bw Selemani Mbacha amesema, wametoa taarifa za awali kwa uongozi wa wilaya hiyo na sasa wanafanya tathmini ya athari za mafuriko ikiwemo hasara na mahitaji halisi ya wananchi.

No comments:
Post a Comment