Image result for yanga
Mechi iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu zaidi katika Azam Sports Federation Cup imemalizika Uwanja wa Namfua kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 kwa njia ya matuta dhidi ya Yanga.
Mchezo huo wa hatua ya robo fainali ya mashindano hayo ulianza kwa kasi huku timu zote mbili zikipambana kupata bao la mapema.
Yanga ndiyo ilikuwa ya kwanza kujipatia bao lililofungwa na Yusuph Mhilu kufuatia mpira wa kona uliopigwa na Ibrahim Ajib kwenye dakika ya 24.
Bao hilo lilifanya dakika 45 za kwanza kumalizika huku Yanga wakiwa kifua mbele kwa goli moja.
Kipindi cha pili kilianza huku Singida wakionekana kulikamia zaidi lango la Yanga, ambapo katika dakika ya 47, Ken Ally, alisaawazishia Singida United kwa bao safi lililofanya mpaka dakika 90 zinamalizika matokeo yakiwa 1-1.
Baada ya dakika 90 kumalizika, hatua ya matuta ilifuata na Singida wakaweza kuibuka kidedea kwa ushindi wa penati 4-2 dhidi ya Yanga hivyo kuwafanya kuingia moja kwa moja katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga iungane na Njombe Mji FC, Tanzania Prisons pamoja na Azam FC zilizoondolewa kwenye hatua hiyo ya robo fainali huku Singida ikiungana na JKT Tanzania, Mtibwa Sugar pamoja na Azam FC zilizotinga kuingia hatua ya nusu fainali.

YANGA YAKUBALI YAISHE, YAKUBALI SHOO YA WALIMA ALIZETI SINGIDA UNITED, NJE RASMI KOMBE LA SHIRIKISHO

No comments:

Post a Comment