Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa,
Charles Kabeho amewaagiza Wahandisi wa Halmashauri kusimamia na
kuzingatia mpangilio uliowekwa katika ramani ya majengo ya miradi ya
Serikali, inayojengwa kwa kutumia fedha za ndani ili kuhakikisha majengo
yanayojengwa yanakuwa ni yenye ubora na yanayodumu muda mrefu.
Rai hiyo aliitoa jana katika kijiji cha Kalinzi kata ya Kalinzi wilaya ya Kigoma Vijijini mkoani Kigoma baada
ya kutembelea jengo la kituo cha afya na kubaini ujenzi huo
haujazingatia vigezo vya serikali na umejengwa chini ya kiwango.
Hali hiyo ilisababisha kiongozi huyo
kukataa kuweka jiwe la msingi katika mradi huo unao tarajiwa kujengwa
kwa kiasi cha shilingi milioni78, na kuwahudumia zaidi ya wananchi elfu
27 wa kata ya Kalinzi.
Kiongozi huyo alisema Mhandisi wa
halmashauri ya wilaya ya Kigoma Ujiji ametumia nondo nne katika jengo
ambalo lilihitajika kuwekewa nondo nane kutokana na sababu zake binafsi
na ujenzi wa jengo hilo lilitakiwa kuzingatia ujenzi huo na kupelekea
kukataa kuweka jiwe la msingi katika mradi wa kituo cha afya na kutoa
msisitizo kwa wahandisi kufuata maelekezo ya mradi na kuomba ushauri kwa
wahandisi wengine ili kuweza kujenga majengo yenye ubora.
"Unaweza kuona ramani ina mapungufu
niwashauri wahandisi jitahidini kuuliza kwa wahandisi wengine ili muweze
kujenga majengo yenye ubora na ya kudumu muda mrefu hatakama jengo
lako nyumbani huwezi kujenga kwa kutumia nondo tatu kutokana na mzigo
uliobebwa na jengo hili Mhandisi hujatendea haki jengo hili simaanishi
tusipo weka jiwe la msingi halitaendelea au watu hawatapata huduma,
hapana hili ni fundisho kufuatilia viwango vinavyohitajika.
"Niombe Mkuu wa wilaya ulisimamie hili,
sisi kama Mwenge wa Uhuru tumeonelea uwekaji wa jiwe la msingi
halitawekwa na mwenge wa uhuru litawekwa kwa utaratibu mwingine",
alisema Kiongozi wa Mbio za Mwenge.
Kwa upande wake Mhandisi wa Halmashauri
ya wilaya ya Kigoma Vijijini, Michael Ntambala alisema yeye kama
mhandisi mshauri wa mradi huo atahakikisha anasimamia mradi huo
marekebisho yote yaliyotolewa na viongozi wa mbio za mwenge na kwamba
walitumia nondo nne kwa kuwa jengo walilojenga halina uzito mkubwa na
kwamba atashirikiana na wahandisi wengine kuona suala hilo wanalitatua.
Nao baadhi ya wananchi kata ya Kalinzi
walisema Kituo hicho cha Afya kimejengwa kwa nguvu za wananchi na
wamekuwa wakijitolea sana na serikali ilichangia fedha na hela nyingine
zilitoka kwa Wafadhili na wao kama wananchi wanatamani sana kuona mradi
huo umekamilika na kuushukuru mwenge wa uhuru kupita na kuibua
mapungufu yaliyopo katika miradi hiyo na kwamba anahakika mradi huo
utarekwbishwa kutokana na maelekezo.
Walisema wananchi hawana uelewa mkubwa
wala utaalamu wa kufanya miradi inayotekelezwa na serikali na kuwaomba
wahandisi kusimamia maelekezo yanayotolewa katika miradi ilikuhakikisha
mradi unakamilika kwa wakati na kutumia mafundi ambao watajenga
majengo yenye ubora na wananchi waendelee kupata huduma karibu.
No comments:
Post a Comment