Kutoka
nchini Kenya Mhifadhi wa Tembo Daphne Sheldrick amefariki dunia kwa
maradhi ya saratani akiwa na umri wa miaka 83, jana April 13, 2018.
Alisaidia
kuokoa maisha ya tembo zaidi ya 230 wengi wao ambao walipoteza mama zao
kwa ujangili au ukame kwa kutengeneza mpango maalumu wa kuwapatia
maziwa na kufanikiwa kwa ufanisi.
Daphne
alizaliwa na kukulia nchini Kenya, alitumia takribani nusu ya miaka
yake ya kwanza kazini, akifanya kazi pamoja na mume wake ambaye alikuwa
Mwingereza David, ambaye ndiye aliyegundua Hifadhi ya Taifa Tsavo
Mashariki nchini Kenya.
Baada
ya kifo cha mumewe mwaka wa 1977, alianzisha mfuko wa David Sheldrick
Wildlife Trust (DSWT), ambao unajulikana zaidi kwa kuokoa na kuimarisha
tembo yatima porini.
Ilimchukua miaka yake 28 kufanikiwa kutengeneza formula maalum ya kunyonyesha tembo kwa maziwa ya chupa.
No comments:
Post a Comment