Waumini wa kanisa la Katoliki katika Dayosisi ya Jimbo la Bungoma nchini Kenya, wako kwenye maombolezo baada ya mchungaji wao kuanguka na kufa papo hapo akiwa madhabahuni.
Kwa mujibu wa Askofu Mkuu wa Jimbo hilo la Bungoma, Norman Kong’oo Wambua, marehemu alianguka majira ya saa 8 mchana katika kanisa la Mabanga ma dakika chache mbele akatangazwa kuwa ameshafariki.
Inaelezwa kuwa kiongozi huyo alikuwa na maradhi ya figo ambayo
wanahisi ndio yaliyosababisha kifo chake cha ghafla. Mwili
umekwisha hifadhiwa mortuary ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.
No comments:
Post a Comment