Marufuku ya matumizi ya adhana (wito kwa waislamu wa kuingia
misikitini kuswali maombi) katika tarafa moja ya mji wa Kigali nchini Rwanda
imepingwa vikali na baadhi ya waislamu jijini humo.
Utawala katika tarafa ya Nyarugenge kunakopatikana jamii
kubwa ya waislam nchini humo, umebainisha kuwa kumekuwepo kwa muafaka wa
kubadili mbinu za kuwaita waumini bila ya matumizi ya njia hiyo ambayo inatajwa
kuwasumbua wananchi.
Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC wa mjini Kigali, John Gakuba
amesema wito huo wa waislamu kuhudhuria maombi umetajwa kuwa kero miongoni mwa
wananchi.
Tayari mkataba wa kuhakikisha kuwa mwafaka huo unaheshimiwa
umetiwa saini kati ya viongozi wa msikiti na utawala wa eneo hilo.
No comments:
Post a Comment