Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo amewafuta kazi Majenerali 18 wa kijeshi nchini humo.
Aidha, inaripotiwa kuwa hatua hii inalenga kusafisha jeshi la nchi hiyo katika mchakato wa kubadilisha mfumo wa usalama.
Rais Farmajo ameamua kwenda kufanya kazi akiwa ndani ya Wizara ya Ulinzi, kuongoza mabadiliko hayo.
Haya ni maamuzi yanayochukuliwa wakati huu serikali ya Somalia ikiendelea kukabiliana na ukosefu wa usalama kutokana na kuwepo kwa kundi la kigaidi la Al Shabab.
No comments:
Post a Comment