Rais John Magufuli amewataka Wahubiri na
Maaskofu nchini Tanzania kwa pamoja kuliombea na Taifa na kuwashawishi
wananchi wake suala zima la kutambua umuhimu wa kujenga viwanda vya
madawa ili kuweza kuzalisha bidhaa zake na kuwapatia vijana ajira.
Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo leo
Machi 26, 2018 wakati alipokuwa anafanya uzinduzi wa magari mapya 181 ya
kusambaza dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara eneo la Keko
Jijini Dar es Salaam.
"Uchumi wa Viwanda hauwezi kufikiwa
bila kuimarisha sekta ya afya, tunatenga bilioni 260 kununua dawa lakini
ni 6% tu ndiyo zinanunuliwa ndani. Tengenezeni njia ya kupata
wawekezaji watakaojenga viwanda vya dawa na vifaa tiba hapa nchini,
sijui watanzania tumerogwa au shetani amekaa mno hapa, basi tumkemee kwa
majina yote akashindwe...
"Ili kusudi watanzania tujue ni namna
gani tunatakiwa kwa kupata fedha. Niwaombe Maaskofu walihubiri na
kulikemea hili na watu wengine wanaojua kuhubiri vizuri tuwaeleza
watanzania kwamba tunapoteza bilioni 500 kila mwaka kununua madawa
wakati tungekuwa tunatengeneza nchini zingebaki hapa,tunalalamikia
mengine yale ya maana ya kuyalalamikia hatuyapigii kelele", amesema Dkt. Magufuli.
No comments:
Post a Comment