
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binaadamu
imekubali hoja 3 kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu katika kesi ya
Babu Seya ikiwemo hoja ya Nguza Viking kutaka apimwe nguvu za kiume.
Akisoma hukumu kwa niaba ya majaji
wenzake, Jaji Gerard Niyungeko aliainisha kwamba kati ya haki
zilizokiukwa wakati wa mwenendo wa kesi hiyo ni ombi la Nguza Viking
kupimwa kitabibu ili kuthibitisha kama hakuwa na nguvu za kiume na hivyo
asingeweza kufanya vitendo vya ubakaji.
Mahakama hiyo imekubali pia hoja kwamba
Viking (maarufu kama Babu Seya) na mwanaye, Johnson Nguza (maarufu kama
Papii Kocha) hawakupata maelezo ya mashahidi wala fursa ya kuwahoji
walotoa ushahidi ili kuthibitisha makosa.
Hata hivyo, hoja nyingine mbalimbali
ziliwekwa kando ikiwemo hoja ya watuhumiwa hao kutolewa gerezani, huku
mahakama ikisema kwamba tayari wameshatolewa kwa msamaha wa Rais John
Magufuli.
No comments:
Post a Comment