Mahakama Kuu nchini Kenya imeamuru
mwanamke aliyeteswa na kudhalilishwa wakati wa kujifungua hospitalini
alipwe fidia ya jumla ya dola 25,000 za Marekani.
Mwanamke huyo
alidhalilishwa miaka mitano iliyopita katika kisa ambacho kilizua lalama
kutoka kwa raia na watetezi wa haki za kibinadamu baada ya kuangaziwa
kwenye vyombo vya habari na mtandaoni.
Jaji wa mahakama kuu ya
Bungoma, magharibi mwa Kenya, Abida Aroni alisema mamlka ya afya nchini
Kenya ilikiuka haki za kimsingi za Josephine Majani alipotengwa na
kukosa kuhudumiwa wakati wa kujifungua katika hosipitali ya umma mwaka
2013.
Jaji huyo alisema kuwa haki za kimsingi za afya za Bi
Majani, pamoja na heshima yake vilikiukwa kupitia yeye kuteswa kimwili
na kutusiwa na wauguzi katika hospitali ya Bungoma.
Na kutokana na hilo, akaamuru alipwe fidia ya dola alfu 25.
Bi Majani amefurahia uamuzi huo akisema kuwa haki hatimaye imetendeka.
Aliyoyapitia
Josephine mikononi mwa wauguzi hao yalipata kujulikana baada ya mtu
kurekodi video kwenye simu yake na kuipakia kwenye mtandao wa kijamii.
No comments:
Post a Comment