Image result for unicef
Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema licha ya watoto wengi kutumia mtandao, kuna juhudi ndogo tu zinazofanywa kuwalinda watoto hao na hatari za dunia ya kidijitali pamoja na kuongeza upatikanaji wa maudhui salama ya mtandao wa internet.
Kwenye ripoti yake ya kila mwaka shirika hilo limesema mmoja kati ya watuamiaji watatu wa mtandao duniani ni mtoto. Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Bw. Anthony Lake amesema katika dunia ya kidijitali, changamoto kubwa ni namna ya kupunguza madhara na kuongeza manufaa ya internet kwa watoto.
Ripoti hiyo imeonesha jinsi teknolojia ya kidijitali inavyoweza kuwa na manufaa kwa watoto wenye matatizo, ikiwemo kuongeza upataji wao wa taarifa, na kujenga ujuzi wa kufanya kazi maeneo ya dijitali, na kuwapa jukwaa la kuungana na kuwasilisha mitazamo yao.

UNICEF latoa wito wa kufanya dunia ya kidijitali kuwa salama kwa watoto

No comments:

Post a Comment