
Mkazi wa Majengo wilayani Kahama mkoani Shinyanga amejinyonga kwa
kutumia kipande cha chandarua usiku wa kuamkia leo akiwa kwenye chumba
chake cha kupanga kwa kile kinachodaiwa kuwa ni ugumu wa maisha.
Kwa mujibu wa kaka wa marehemu Said Ndago amesema kuwa mdogo wake
ambaye amejinyonga anaitwa Jumnne Said Ndago ambaye alikuwa
ameachishwa kazi ya Udreva katika halmashauri ya Msalala kutokana na
kutokuwa na vyeti.
Amesema kuwa kabla ya kujinyonga aliandika Meseji kwa dada yake ambaye
anafanya kazi Jijini Dar es salaam ambayo ilikuwa inasema kuwa
anamuomba amtunzie watoto wake kwani yeye hatakuwepo duniani .
Kwa upande wake jirani wa marehemu ambaye walikuwa wanaishi nyumba moja
Edward Nkondi amesema kuwa kijana huyo hakuwa anashinda Nyumbani
kutokana na kuwa mke wake wake alikuwa amekwenda kwao Tabora hivyo
alikuwa anaishi Peke yake hali ambayo ilikuwa ikichangia kutoshinda
Nyumbani.
Amesema kuwa alikuwa anafika kwake usiku , lakini pamoja na kufika kwake
alikuwa haonyeshi dalili za kwamba angefanya tukio kubwa kama hilo
alilofanya la kujinyonga na kwamba alikuwa kijana mcheshi na mchangamfu.
Naye mkuu wa kitenngo cha Upelelezi ndani ya jeshi la Polisi mjini
Kahama George Bagyemu kwa niaba ya Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga
Simon Haule amekiri kupokea taarifa hiyo na kwamba tatizo la
kujinyonga ni ugumu wa maisha .
No comments:
Post a Comment