Wabunge wa Uganda wameyapitisha
mabadiliko ya Katiba ambayo sasa yanamruhusu Rais wa sasa Yoweri Kaguta
Museveni kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa kwa muhula wa sita.
Baada
ya siku tatu za majadiliano mazito na mivutano, hatimaye waondoa ukomo
wa umri wa miaka 75 kwa mgombea urais. Wabunge wa upinzani walitoka
ndani ya ukumbi zaidi ya mara moja na sita kati yao walifukuzwa ukumbini
kutokana na kuupinga muswada.
Na hatimaye spika wa bunge hilo Bi
Rebecca Kadaga akitangaza matokeo baada ya kupiga kura ya mwisho ikiwa
wapiga kura wawili hawakuwa na upande, upinzani wamepata kura 62 na
wanaotaka kuondowa kikomo kura 315 na hivyo Spika kutangaza kuwa mswaada
huo umepita baada ya kusomwa mara ya tatu.
Wabunge pia wamerejesha ukomo wa vipindi viwili vya kukaa madarakani
kutoka miaka saba hadi miaka mitano, kwa hivyo wabunge wa sasa
wataendelea kuongoza hadi mwaka 2023.
Ni pengine kutokanana
malalamiko kuwa kuondolewa kwa ukomo wa umri kunaweza kumfanya Bwana
Museveni kuwa Rais wa milele. Wafuasi wa Museveni wanadai ni waganda
ndiyo wanaweza kumwondoa madarakani kwa Kura.
Upande wa upinzani waliweka pingamizi kuzuia mswaada huo usipite
lakini idadi yao katika bunge ni ndogo, kiongozi wa wabunge wa upinzani
Winne Kiiza amesikitishwa na kupitishwa mswaada huo.
Lakini upande wa chama tawala ulitumia kila mbinu kuona kwamba mswaada huo unapita ili Rais Museveni kuendelea kutawala .
Kupitishwa
mswaada huo kunampatia tena Rais Museveni kutawala miaka mingine 14
kulingana na mswaada huo, lakini raia wa Uganda wengi walikuwa hawaungi
mkono kubadilishwa kwa katiba kumuongeza Rais Museveni kutawala baada ya
kutawala zaidi ya miongo mitatu.
No comments:
Post a Comment