Taarifa za hivi
punde ni kwamba Singida imeimarisha safu ya Ushambuliaji kwa kuongeza
washambuliaji Kambale Salita (Papy Kambale) na Danny Lyanga huku
wachezaji wawili wakitalajiwa kutangazwa hivi punde.
Katika hatua za
kuendeleza mpira nchini, klabu ya Singida United imewasaka na kuwapata
vijana wanne walioshiriki Michuano mikubwa barabi Africa kwa vijana umri
chini ya miaka 17 AFRICON 2017 waliokuwa na kikosi cha Serengeti Boys.
Hatua hiyo ni moja ya
mipango iliyowekwa na uongozi wa kusaidia vijana hasa wale ambao
walishaonekana na hata kulipigania Taifa na baada ya michuano hiyo
kumalizika wengi wao walitawanyika na kukosa timu za kusimama nao.
Hivyo katika kulinda
vipaji hivyo, Singida United imeamua kuchukua wachezaji wa nne kwa
usajili wa miaka mitatu kila mmoja huku wakilipwa Signing fee,mshahara
na allowance stahiki zao ili kuwajenga katika mfumo wa soka la
ushindani.
Vijana hao,mmoja
ni kepteni wa Serengeti Boys Ndg.Issa Makamba kiungo wa kati,Mwingine ni
Assad Juma mshambuliaji nimzaliwa wa Zanzibar, pia Ally Ng’azi beki na
Mohamed Abdallah mshambuliaji.
No comments:
Post a Comment