Kundi la wanawake katika Mtaa Majengo
wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamemshambulia kwa kumpiga mkazi wa
mtaa huo aliyefahamika kwa jina la Andrew baada ya kwenda na mwanamke
mwingine nyumbani kwake na kumtaka mke wake awapishe kitandani ili
walale.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo ambapo majirani hao walifikia
hatua hiyo baada ya kuamshwa na kelele zilizokuwa zikiendelea baina ya
wanandoa hao.
Akizungumza na Kahama fm, Mke wa mwanaume huyo, Mariam Abdallah, (32)
amesema mume wake alifika usiku majira ya saa tano akiwa na mwanamke
huyo ambapo alimtaka awapishe kitandani ili walale na yeye akalale
sebuleni.
Hata hivyo baada ya kuona hivyo walianza malumbano ndipo majirani
walipofika na kuanza kumshambulia mume wake wakisema amewadharirisha
wanawake wa eneo hilo.
Kwa upande wake mume wa Mke huyo bwana Andrew amesema mwanamke huyo ni
mke wake wa pili, na kwamba alifika nyumbani kwa lengo la kujiandaa
kwenda kumpokea mama yake mzazi aliyekuwa anatoka Dar es Salaam ambapo
wangeenda wote watatu kwa kuwa alishawatambulisha.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha dawati la jinsia na watoto kutoka
jeshi la Polisi wilayani Kahama, Gumba Mipawa amethibitisha kutokea
tukiko hilo na kwamba wanaendelea kuwahoji wanandoa hao.
Kwa mujibu wa kitengo cha dawati la jinsia wilayani humo, hilo ni tukio
la kwanza kuripotiwa kwenye kitengo hicho tangu kianzishwe wilayani
humo.
No comments:
Post a Comment