Aliyekuwa mkuu wa jeshi nchini Zimbabwe Constantin Chiwenga ameteuliwa kuwa makamu mpya wa rais wa Zimbabwe.
Alistaafu hivi majuzi na kuwa naibu wa chama tawala cha Zanu-Pf mnamo Disemba 23.
Naibu mwengine wa chama tawala cha Zanu-Pf ,aliyekuwa waziri wa maswala ya kigeni nchini Zimbabwe Kembo Mohadi pia atateuliwa kuwa makamu wa rais.
Rais mpya Emmerson Mnangagwa alichukua mamlaka baada ya jeshi kuingilia kati mnamo tarehe 15 mwezi Novemba kufuatia mgogoro wa kumrithi Robert Mugabe.
Siku chache kabla ya jeshi kuchukua mamlaka , bwana Mnangagwa , wakati huo akiwa naibu wa rais alifutwa kazi na kuondoka nchini humo katika kile kilichoeleweka kuwa jaribio la rais kumpatia uongozi mkewe Grace kuwa mrithi wake.
No comments:
Post a Comment