Na Method Charles
Papa mtakatifu Francis amekuwa kiongozi wa kwanza wa kanisa la katoliki kuunga mkono sheria za watu wa jinsia moja.
Papa Francis siku ya jumatano aliitisha kupitishwa kwa sheria za watu wa jinsia moja akitofautiana na msimamo wa muda mrefu wa kanisa hilo kuhusu suala la ndoa za jinsia moja
“Wapenzi wa jinsia moja wana haki ya kuwa sehemu ya familia watoto wa Mungu na hawafai kutupwa nje au kunyanyaswa kwa ajili ya mahusiano yao’ amesema Papa Francis.
Francis hapo awali alikuwa ameunga mkono ndoa za watu wa jinsia moja alipokuwa Askofu mkuu wa Buenos Aires.
Matamshi hayo yake yanatarajiwa kuzua mjdala miongoni mwa waumini wa kanisa la katoliki.
Hata hivyo ametolea Mfano mtoto akiwa jambazi huwezi kumkana kuwa si mwanao atabakikuwa mwanao kinachotakiwa ni kumuelimisha taratibu aache tabia hiyo.

No comments:
Post a Comment