PROFESSOR ZEMSHAMBA : BILA ELIMU UPAKO NI BURE

 Imeelezwa kuwa Wachungaji wengi wamekuwa hawana utaalamu wa kufanya kazi ya Mungu badala yake wamekuwa wakitegemea upako bila kuwa na elimu ambayo ita wasaidia kufikisha ujumbe kwa jamii.

Hayo yamesemwa na Mkufunzi wa Chuo cha Japanese Bible Institute Professor Paul Zemshamba wakati wa Mahojiano Maalum na Habari Maalum Media.

Amesema Ilikuweza kufikisha ujumbe unaotakiwa ukiwa katika Hali ya Kitaalamu na Usahihi mchungaji anatakiwa kuwa na elimu ili kuepuka Ukanjanja.

Professor Zemshamba amesema kwa Kufanya Hivyo Upako unatakiwa kuendana na Elimu inayowiana

"upako pekee hautoshi inahitajika elimu na ujuzi ili kuwa na mpangilio mzuri wa masomo badala ya kuhubiri masomo mengi kwa wakati mmoja kwa jamii na kuchanganya watu wasiweze kujifunza vizuri" Alisema Professor Zemshamba

 

No comments:

Post a Comment